Enrolment options
Katika kozi hii ya mafunzo binafsi, utajifunza namna ya kuwa Mdadisi wa Kidigitali (Digital Enquirer): mtu anayefahamu namna ya kutambua Taarifa Potofu, kupata, kukusanya na kuchambua taarifa sahihi mtandaoni, na kuisambaza katika namna salama.
Kozi hii ni ya kwa ajili ya nani? Watumizi wa teknolojia za kidigitali wanaotamani kuweka usalama zaidi katika nyanja ya taarifa na mawasiliano. Iwe wewe ni mwanaharakati wa kijamii, mtetezi wa haki za binadamu, (raia) mwandishi wa habari, au iwe unajaribu tu kupekua taarifa mtandaoni, hii ni kozi sahihi kwa ajili yako!
Utajifunza nini?
>
Kutambua na kujibu taarifa potovu.
>
Kuhakiki taarifa za mtandaoni na mambo msingi ya uthibitisho
>
Kufanya kazi kwa usalama na kulinda taarifa
>
Kutambua namna ya kujilinda na kuwalinda wengine
Unahitaji kuwekeza muda kiasi gani? Kila moduli inajumuisha masomo kadhaa, ambayo kila moja wapo huchukua dakika 15. Hili linamaanisha kwamba, moduli moja itachukua takribani dakika 90 kukamilika.
Utapokea cheti cha aina gani? Cheti cha ushiriki kwa kila moduli, baada ya kuhitimu
Kozi hii ilitengenezwa na Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH kwa kushirikiana na Tactical Tech
Leseni: Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0 International (CC BY-SA 4.0), Tactical Tech na GIZ.