Nyenzo ya Mdadisi wa Kidijitali (Digital Enquirer Kit)

Katika
kozi hii ya mafunzo binafsi, utajifunza namna ya kuwa Mdadisi wa
Kidigitali (Digital Enquirer): mtu anayefahamu namna ya kutambua Taarifa
Potofu, kupata, kukusanya na kuchambua taarifa sahihi mtandaoni, na
kuisambaza katika namna salama.


Kozi hii ni ya kwa ajili ya nani?  Watumizi
wa teknolojia za kidigitali wanaotamani kuweka usalama zaidi katika
nyanja ya taarifa na mawasiliano. Iwe wewe ni mwanaharakati wa kijamii,
mtetezi wa haki za binadamu, (raia) mwandishi wa habari, au iwe
unajaribu tu kupekua taarifa mtandaoni, hii ni kozi sahihi kwa ajili
yako!

                         

Utajifunza nini?


Kutambua na kujibu taarifa potovu.


Kuhakiki taarifa za mtandaoni na mambo msingi ya uthibitisho

Kufanya kazi kwa usalama na kulinda taarifa

Kutambua namna ya kujilinda na kuwalinda wengine

Unahitaji kuwekeza muda kiasi gani? Kila moduli inajumuisha masomo kadhaa, ambayo kila moja wapo huchukua dakika 15. Hili linamaanisha kwamba, moduli moja itachukua takribani dakika 90 kukamilika.  

Utapokea cheti cha aina gani? Cheti cha ushiriki kwa kila moduli, baada ya kuhitimu

Kozi hii ilitengenezwa na  Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH kwa kushirikiana na  Tactical Tech 
Leseni: Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0 International (CC BY-SA 4.0), Tactical Tech na GIZ.