Kupambana na Dhuluma za Kijinsia Mtandaoni - Digital Enquirer Kit

Katika mafunzo haya ya mtu binafsi, utajifunza namna ya
kutambua na kupambana na dhuluma za kijinsia mtandaoni (OGBV).

Kozi hii ni sehemu ya Nyenzo ya Mdadisi wa Kidijitali (Digital
Enquirer Kit), ambao ni mwongozo wa mafunzo ya mtandaoni ya kutambua taarifa potovu
na namna ya kuthibitisha taarifa za kuaminika, huku ukidumisha usalama wako
mtandaoni. Tazama mafunzo yetu ya mtandaoni yanayopatikana kwenye Nyenzo ya
Mdadisi wa Kidijitali (Digital Enquirer Kit)hapa.

          Kozi hii ni kwa ajili ya nani?Kozi
hii imeundwa mahsusi kwa ajili ya wanawake (na wale wote wanaojitambulisha kama
wanawake); wanawake mashuhuri, watu wa jamii ya wasagaji, mashoga, wanaovutiwa
kimapenzi na jinsia zote mbili, waliobadili jinsia, mahuntha na kadhalika
(LGBTIQ+), wanaharakati wa kijinsia, na watetezi wa haki za binadamu. Pia imekusudiwa kugusia watu walioathiriwa na dhuluma za
kijinsia mtandaoni, pamoja na wale wanaotaka kufahamu namna ya kushiriki katika
kuwasaidia waathiriwa hao, au kuingilia kati, kwa njia salama
.

Ifikapo mwishoni mwa kozi hii, utaweza
>  Kueleza namna mahusiano ya
kijinsia yanavyobadili ulimwengu wetu wa kijamii

>  Kutambua kwa nini jinsia inaweza
kuwa chanzo cha dhuluma mtandaoni

>  Kutambua dhuluma za kijinsia
mtandaoni

>  Kutambua mbinu za kujiweka
salama pindi unapoanza kubuni ujumbe wako mtandaoni

Kujilinda na kuwavutia washirika au marafiki wa
kukusaidia mtandaoni

Unahitaji kutumia muda kiasi gani?
Kozi hii inajumuisha vipindi sita, kila kimoja kikichukua kati ya dakika
10-20. Hili linamaanisha kwamba, itakuchukua takribani dakika 90 kukamilisha
kozi yetu inayohusu dhuluma za Kijinsia Mtandaoni.

Utapokea cheti cha aina gani? Cheti cha ushiriki kwa kila moduli, baada ya kuhitimu

*Kwa ufikivu usio wa kimtandao, pakua Programu ya atingi (ipatikanayo kwa ajili ya Android katika Stoo ya Google Play).*

Kozi hii ilitengenezwa na shirika la Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH kwa ushirikiano naKICTANet naTaasisi ya Masomo ya Jinsia na Ustawi katika Chuo Kikuu
cha West Indies, Barbados (UWI)
.
Leseni:‘Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0
International (CC BY-SA 4.0)’, ‘KICTANet’, ‘UW’I na ‘GIZ’
. Picha zilizotiwa alama ifuatayo "CC
BY-NC-ND" zinaweza kutumika katika muktadha/mazingira ya mafunzo haya ya
mtandaoni, sifa za hakimiliki zikielekezwa kwa mbunaji au mchoraji wa picha
hizi, ila tu kwa madhumuni yasiyokuwa ya kibiashara.

sdfsdfgiz